Saturday, January 12, 2013

Leo hii Mungu ameweka neno hili moyoni mwangu nalo natamani ulisome. Luka 2:21. Neno linasema- Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. 
          Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa damu ya Yesu kumwagika. Wakati akitahiriwa damu yake ilimwagika na kuwa uashirio wa Agano jipya. Nasema ni uashirio wa agano jipya kwa sababu Yesu alitahiriwa kwa sababu ya agano ambalo Mungu mwenyewe aliliweka kupitia kwa Ibrahimu. Soma Mwanzo 17:1-14. Naomba niandike mistari kadha kwenye habari hiyo lakini ningependa usome mwenyewe habari yote. Mstari wa nne Imeandikwa. Mimi, agano langu nimelifanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,............Mstari wa sita imeandikwa. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.....Mstari wa kumi unasema. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, kila mwanaume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. 
           Kwa hiyo Yesu naye kwa kuwa alikuwa ni Myahudi ilimpasa kutahiriwa, ili atimize agano la Mungu alilofanya na Ibrahimu. Lakini tofauti kubwa yeye ni Mungu aliyevaa mwili wa kibinadamu na kuitwa Yesu. kwa nini amwage damu yake (wakati wa kutahiriwa) kutimiza agano la mungu? Kwanza agano ni ahadi au mkataba. Mungu aliweka ahadi na Ibrahimu kwa akisema-----UTAKUWA BABA WA MATAIFA MENGI. -----NITAKUFANYA UWE NA UZAO MWINGI SANA, NAMI NITAKUFANYA KUWA MATAIFA. ...............................(ITAENDELEA..............................)


No comments:

Post a Comment